Wanahabari Machakos waapa kuzingatia maadili wakitaka vitisho vikome

Marion Bosire
1 Min Read

Wanahabari kaunti ya Machakos wameapa kutekeleza wajibu wao kwa kufuata maadili ila wanatoa onyo kwamba hawafai kutishiwa wakiwa kazini.

Wakizungumza walipoungana na wenzao katika maandamano ya kitaifa ya wanahabari, aidha wameshtumu asasi mbalimbali kwa kukandamiza uhuru wa wanahabari kama vile serikali, bunge, polisi pamoja na jeshi.

Mdau katika muungano wa wahariri KEG Martin Masai anasema hawahitaji kupendelewa au kubembelezwa kutoka kwa yeyote ila kupewa uhuru wa kuendesha majukumu yao kwa kuwa hawaegemei upande wowote.

Masai anasema wanahabari wamepitia wakati mgumu wakati wa kupeperusha matukio ya maandamano nchini na iwapo mwanahabari atashambuliwa inamaanisha mkenya ananyimwa fursa ya kupata habari.

Kauli yake imeungwa na mwenzake wa shirika la Standard Group Rose Mukonyo anayeshangaa ni kwa nini mwanahabari wa kike amekuwa kifaa cha kuelekezewa mashambulizi ilhali kazi ya wanahabari ni kuripoti matukio jinsi yalivyo.

Aanasisitiza kuwa wanahabari hawaegemei upande wowote na kuwashambulia ni kinyume cha sheria.

Mwenzao wa runinga ya Citizen Enock Muswi anasema inawatia hofu kutekeleza wajibu wao wakati wanaposhuhudia wenzao wakishambuliwa huku polisi wakitazama.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *