Wanafunzi wa kike wanawiri katika Insha ya Kingereza na Lugha ya Ishara

Tom Mathinji
1 Min Read

Somo la Insha ya kingereza na somo la lugha ya  ishara, ziliandikisha matokeo bora zaidi katika mtihani wa mwaka huu wa darasa la nane KCPE.

Akitangaza matokeo ya mwaka huu ya darasa la nane KCPE katika jumba la mitihani Jijini Nairobi siku ya Alhamisi, waziri wa elimu Ezekiel Machogu, alisema wanafunzi wa kike walifanya vyema zaidi katika masomo hayo kuliko wenzao wa kiume.

Hata hivyo Machogu alisema matokeo ya masomo hayo mengine yamedorora ikilinganishwa na yale ya mwaka 2022.

kwa upande mwingine, wanafunzi wa kiume walifanya vyema katika masomo ya hisabati na sayansi, kuliko wenzao wa kike.

Machogu alisema wanafunzi 8,523 walipata alama 400 na zaidi, ikilinganisha na wanafunzi 9,443 waliopata alama 400 na zaidi katika mtihani wa KCPE wa mwaka jana.

Aidha kulingana na waziri huyo, asilimia 51.30 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo walikuwa wakiume huku asilimia 48.70 ya wanafunzi hao wakiwa wa kike.

Wanafunzi 1,406,557 walifanya mtihani wa mwaka huu wa KCPE, ambao ndio wa mwisho kwani umehitimisha mfumo wa elimu wa 8-4-4 huku mfumo mpya wa elimu wa CBC ukianza kutekelezwa.

Website |  + posts
Share This Article