Ni afueni kwa wanafunzi kutoka maeneo yanayokumbwa na wizi wa mifugo nchini, baada ya Rais William Ruto kutangaza kuwa watalipa karo ya shilingi 5,000 pekee kwa mwaka kutoka shiingi 30,000.
Rais alisema haya jana alipoanza ziara yake ya siku tatu katika eneo la North Rift, akisisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule katika kaunti za West Pokot, Baringo na Elgeyo Marakwet.
Ruto alitangaza hayo jana alipozuru kaunti ya Elgeyo Marakwet.