Wanafunzi kadhaa wajeruhiwa baada ya bweni la shule ya upili ya Kibokoni kuteketea

Dickson Wekesa
1 Min Read

Wanafunzi kadhaa katika shule ya upili ya Kibokoni kaunti ya Kilifi wamepata majeraha baada ya bweni la wasichana kuteketea leo Alhamisi asubuhi.

Stembo Kaviha, mmoja wa waliofika shuleni humo, anasema moto huo ulianza kwenye bweni hilo la wanafunzi wa kike na ilichukua muda wa saa mbili kwa wakazi, walimu pamoja na zima moto kuuzima moto huo.

Aidha wanafunzi walikuwa katika hali ya taharuki wakiokoa mali zao kwenye bweni hilo huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.

Stembo aidha ameshutumu vikali hatua ya mwalimu mkuu wa shule hiyo Patrick Mwangi kukataa katakata kuzungumza na wanahabari. Mwangi badala yake aliwaamuru walimu kuwafurusha wanahabari ambao walikua wamefika kwenye eneo la mkasa kuangazia mkasa huo wa moto.

Maafisa wa Shirika la Msalaba mwekundu wamefika katika eneo la mkasa na kuwasaidia kupata huduma ya kwanza wanafunzi ambao wamepata majeraha kabla ya kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Dickson Wekesa
+ posts
Share This Article