Wanafunzi 140,107 waliofanya mtihani wa kidato cha nne, KCSE mwaka uliopita wameteuliwa kujiunga na vyuo vikuu nchini.
Akitoa ripoti hiyo leo Jumatatu, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesema wanafunzi 130,485 wameteuliwa kujiunga na vyuo vikuu vvya umma huku idadi iliyosalia ya 9,622 wakiteuliwa kujiunga na vyuo vikuu vya kibinafsi.
Wanafunzi 144,500 wameteuliwa kujiunga na vyuo vya kiufundi, TVET huku 560 wakijiunga na vyuo vy kutoa mafunzo ya walimu wa sekondari.
Wanafunzi wengine 9,673 waliohitimu kujiunga na vyuo vikuu walihiari kujiunga na vyuo vya TVET.