Wanafunzi 113 wapata ufadhili wa masomo kutoka Benki ya Equity

Dismas Otuke
1 Min Read

Benki ya  Equity imetoa ufadhili wa kima cha shilingi bilioni 2.8 kwa  kwa wanafunzi 113, waliokalia mtihani wa KCSE mwaka uliopita.

Ufadhili huo wa masomo utawawezesha wanafunzi hao waliopata alama ya A, kupokea masomo katika  vyuo vikuu 71  katika mataifa 22 tofauti.

Wanafunzi hao wamepokea ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Afisa Mkuu mtendaji wa benki ya Equity Isaac Mwangi, amesema ana imani wanafunzi hao watabadilisha maisha ya jamii zao.

 

Website |  + posts
Share This Article