Utawala katika mji wa Nyeri umewataka wamiliki wa sehemu za burudani au vilabu vya usiku hasa katika eneo la Kirichu kuzingatia sheria ya uuzaji wa pombe.
Tangazo hili linafuatia mkutano uliofanyika kati ya wakazi wa eneo hilo na maafisa wa usalama baada ya wakazi hao kutishia kufanya maandamano kulalamikia ukosefu wa usalama.
Wanaamini kwamba hali hiyo inasababishwa na vijana ambao hubugia pombe katika vilabu hivyo na baada ya kulewa wanazua vurugu.
Naibu kamishna wa kaunti katika eneo hilo la Nyeri mjini Joseph Mwangi amewahikikishia wakazi wa Kirichu usalama na utulivu akisema kwamba suala la vilabu vya usiku litatatuliwa katika muda wa siku chache zijazo baada ya bunge la kaunti ya Nyeri kupitisha sheria mpya ya kudhibiti vileo.