Wamarekani wapiga kura kumchagua Rais mpya

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha ya Eugene Tanner wa AFP

Mamilioni ya raia wa Marekani leo Jumanne wanapiga kura kumchagua mrithi wa Rais Joe Biden anayeondoka madarakani baada ya kuhudumu kwa muhula mmoja. 

Ushindani ni kati ya mgombea wa chama cha Democrat Kamala Harris na Donald Trump.

Harris kwa sasa anahudumu kama Makamu wa Rais huku Trump akiwa Rais wa zamani wa nchi hiyo.

Jana Jumatatu, wagombea wote wawili walifanya kampeni zao za lala salama katika jimbo la Pennsylvania, moja ya majimbo yenye ushindani mkali na yanayotazamiwa kutekeleza jukumu muhimu katika kuamua mshindi wa uchaguzi huo.

Masuala ya uaviaji mimba, udhibiti wa mipaka na mfumko wa bei yanatazamiwa kuwa na ushawishi mkubwa wa ni nani atayechaguliwa kuiongoza nchi hiyo yenye ushawishi mkubwa duniani.

Trump alipiga kura katika katika jimbo la Florida karibu na makazi yake ya Mar-a-Lago.

Alinukuliwa akisema ana “imani kubwa” na kwamba anataka kuwa mtu “jumuishi kabisa.”

Foleni ndefu za wapiga kura zilionekana katika uchaguzi huo wenye ushindani mkali na unaofuatiliwa kwa karibu duniani kote.

 

 

Share This Article