Idadi ya watu waliouwa nchini Msumbiji kutokana na kimbunga cha Chido imefikia 45 baada ya manusura zaidi kufariki wakipokea matibabu hospitalini.
Kimbunga hicho kilizuka Jumapili iliyopita na kuharibu nyumba zaidi ya 35,000, katika mikoa ya Cabo Delgado and Nampula kaskazini mwa nchini hiyo.
Umoja wa mataifa tayari umetoa misaada ya kima cha dola milioni nne za Marekani huku ikikadiriwa kuwa watu 181,000 waliathirika na kimbunga hicho.