Mke wa naibu Rais mchungaji Dorcas Rigathi, ameanzisha mpango wa majaribio wa upanzi wa mitiunaowahusisha vijana waliokuwa waraibu wa mihadarati.
Mpango huo wa majaribio umeanzishwa katika kijiji cha Kiamariga Village, kaunti ya Nyeri, kabla ya kuzinduliwa katika sehemu zingine za taifa.
Akizungumza alipokuwa akitangamana na vijana walio katika mpango huo, mchungaji Dorcas alisema hadi kufikia sasa mpango huo umewasaidia vijana wengi kusitisha utumizi wa mihadarati.
“Tunataka kuanzisha mpango huo hapa, ukifaulu tutauanzisha katika maeneo mengine ya nchi,” alisema mchungaji Dorcas.
Paul Waihenya mwenye umri wa miaka 22, ni mmoja wa walionufaika na mpango huo, alisema tangu alipojiunga na mradi huo hajatumia mihadarati tena.
” Kabla ya mpango huu nilikuwa natumia aina zote za mihadarati, lakini nyakati hizi sina muda wa mihadarati kutokana na shughuli nyingi nilzo nazo,” alidokeza Waihenya.
Vijana hao wanalenga kupanda miti 500,000.
Mpango sawia na huo unatekelezwa na wajane katika eneo la Loitoktok, kaunti ya Kajiado ukiwa na lengo la kupanda miti 500,000.