Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya barbarani Jumatatu iliyopita katika eneo la Maltauro karibu na Duka Moja , barabara kuu ya Narok-Mai Mahiu imefikia saba.
Ajali hiyo ilitokea wakati ambapo dereva wa lori lililokuwa likitremka mlima wa Nairagie-Enkare, alipopoteza mwelekeo na kugongana na magari kadhaa yakiwemo basi na magari ya kibinafsi.
Zaidi ya watu 20 walijeruhiuwa katika ajali hiyo iliyosababisha msongamano mkubwa wa magari.