Walioangamia kwenye tetemeko la ardhi Morocco yapanda hadi zaidi ya 1,000

Dismas Otuke
1 Min Read

Zaidi ya watu 1,037 wameripotiwa kuaga dunia na wengine 1,200 kurejuhiwa  kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lilitokea nchini Morocco Ijumaa usiku eneo la Marrakech.

Kulingana na kituo cha utafiti na sayanzi ,tetemeko hilo lilozuka mida ya saba na dakika 11 usiku wa manane katika mkoa wa Al-Haouz, kusini mashariki mwa mji wa Marrakech,ulio maarufu kwa kuwa na idadi kubwa ya watalii.

Watu 820 wanaamika kufariki na wengine 672 kujeruhiwa vibaya kulingana na taarifa kutoka kwa wizara ya usalama wa kitaifa .

Mataifa ya Ufaransa,Marekani na Uturuki ni baadhi ya washirika waliojitolea kuisadia Morocco kutuatia mkasa huo ambao ndio mbaya zaidi kutokea nchini humo.

Eneo la Marrakesho lina idadi ya watu zaidi ya milioni 1 nukta 8 wanaoishi .

TAGGED:
Share This Article