Tume ya kuwaajiri Walimu nchini (TSC) imetoa ilani mpya inayowashurutisha walimu wakuu wa shule za upili na manaibu wao katika mtaala wa umilisi (CBC) wawe na shahada ya uzamili.
Aidha, walimu wakuu wa shule za msingi watalazimika kuwa na shahada ya ualimu ili kuhudumu kwenye wadhifa huo.
Kwenye taarifa iliyowasilishwa na TSC kwa kamati ya elimu ya bunge la Seneti mapema mwezi huu, walimu wanaotaka kuwa walimu wakuu waandamizi watahitajika kuwa wamehudumu katika nyadhifa za naibu mwalimu mkuu au katika nafasi sawia kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
Pia, walimu wanaotaka nafasi za naibu mwalimu mkuu lazima wawe wamehudumu katika nafasi za mwalimu mwandamizi kwa zaidi ya miaka mitatu.