Walimu wa JSS kuajiriwa kuanzia Julai 1 mwaka huu

Dismas Otuke
1 Min Read

Walimu wa Junior Secondary School walioajiriwa kwa  mkataba  mfupi Januri mwaka huu, wataajiriwa kwa mkataba wa kudumu kuanzia Julai mosi mwaka huu.

Hii ni baada ya bunge la kitaifa kuingilia kati na kuamrisha walimu hao 26,000, waliokuwa wameajiriwa kama wanagenzi na mikataba mifupi wapewe kandarasi za kudumu.

Walimu hao wamekuwa wakigoma tangu shule zilipofunguliwa kwa muhula wa pili mwezi huu, kupinga arifa ya tume ya kuwaajiri TSC ya kupewa mikataba ya kudumu kuanzi Januari mwakani.

TAGGED:
Share This Article