Walimu wa JS Lamu wataka shule hizo ziwe huru

Marion Bosire
1 Min Read

Walimu wa Shule za Sekondari msingi – JS katika kaunti ya Lamu wamejiunga na wenzao kote nchini kushinikiza Wizara ya Elimu kutenganisha usimamizi wa JS na ule wa shule za msingi.

Wakiongozwa na Edward Mbuthi, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari na Vyuo – KUPPET tawi la Lamu, walimu hao wanadai kuwa kutenganisha mifumo ya kifedha na bodi za usimamizi kati ya viwango hivi viwili kutaboresha utendakazi wa walimu wa JS na kuinua matokeo ya wanafunzi.

Wakati huo huo, Ayub Were, mpinzani wa Mbuthi katika uchaguzi ujao wa nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa KUPPET tawi la Lamu, amewashutumu viongozi wa chama hicho waliokutana na Rais William Ruto mapema wiki iliyopita kwa kushirikiana na serikali kukandamiza maslahi ya walimu wa JS.

Website |  + posts
Share This Article