Walanguzi watatu wa Mihadarati wanaswa Mombasa na Kilifi

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wa mihadarati wanaswa Pwani ya Kenya.

Maafisa wa polisi wa kitengo cha kukabiliana na mihadarati, wamenasa dawa za kulevya za thamani ya shilingi milini 3.7, baada ya kufanya msako katika kauni ya Mombasa na Kilifi.

Katika msako huo uliotekelezwa May 7, 2024, gramu 50 za Cocaine na kilo 1.15 za heroine zilipatikana.

Katika mtandao wake wa X, idara ya uchunguzi wa maswala ya Jinai DCI, ilisema mshukiwa Hussein Mansur Salim, alikamatwa katika eneo la  Kisauni, Mwandoni akiwa na gramu 50 za cocaine, thamani ya shilingi 250,000.

Katika kituo cha magari cha Stage ya Paka, Ali Swale alitiwa nguvuni akiwa na kilo moja ya ya heroin ya thamani ya shilingi 3,000,000.

Wakati huo huo, Harrison Mwenda Kiambi alinaswa katika eneo la Mtwapa Maweni akiwa na gramu 150 ya heroin, ya thamani ya shilingi 450,000.

Kulingana na DCI, washukiwa hao watatu wanazuiliwa na polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article