Wakulima waunga mkono kuahirishwa kwa uchaguzi wa Bodi ya Sukari nchini

Martin Mwanje
1 Min Read

Wakulima wa miwa magharibi mwa nchi wameunga mkono uamuzi wa Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe kuahirisha uchaguzi wa Bodi ya Sukari nchini, KSB.

Uchaguzi huo ulikusudiwa kuandaliwa Sptemba 5 mwaka huu.

Uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na kesi kadhaa zilizowasilishwa mahakamani kuupinga.

Wakizungumza nje ya Mahakama ya Busia, wakulima hao wakiongozwa na Monica Mong’ala walisema kesi zilizowasilishwa mahakamani ni muhimu katika kubaini ustahiki wa wagombea wanaotaka nyadhifa za ukurugenzi.

Walidai baadhi ya wagombea waliotarajiwa kugombea waliondolewa kwenye orodha na kutilia shaka usawa na uaminifu wa mchakato wa uchaguzi.

Sasa wanaitaka Wizara ya Kilimo na washikadau wote kuhakikisha uchaguzi huo unafanywa kwa njia ya haki, uwazi na jumuishi punde kesi zilizowasilishwa mahakamani zitakapoamuliwa.

Share This Article