Wakulima wataka serikali iongeze bei ya mahindi hadi shilingi 6,000

Dismas Otuke
1 Min Read
Katibu katika wizara ya Kilimo Dkt. Paul Rono.

Wakulima wameitaka serikali kuongeza bei ya kununua mahindi kutoka shilingi 4,000 hadi 6,000, kwa gunia la kilo 90 kutoka kwa wakulima.

Wamehoji kuwa bei mpya iliyotangazwa na halmashauri ya nafaka na mazao
NCPB, huenda ikachangia wakulima kupata hasara kutokana na bei ya juu ya kununua  pembejeo.

Hata hivyo huenda kilio cha wakulima hao kikawa kelele za chura mtoni, baada ya Katibu katika Wizara ya Kilimo Paul Ronoh, kutangaza wiki jana kuwa serikali haina uwezo na nia ya kuongeza bei ya zao hilo.

Wakulima kutoka maeneo ya North Rift yanayokuza mahindi kwa wingi wanatarajiwa kuanza kuvuna kaunzia mwezi ujao.

TAGGED:
Share This Article