Wakulima walilia mbegu za mahindi West Pokot

radiotaifa
1 Min Read

Taarifa ya Stephen Ayiengo

Baadhi ya viongozi na wakulimaa kaunti ya Pokot Magharibi wametoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo kuharakisha usambazaji wa mbegu za mahindi zinazotolewa bila malipo kwa familia zisizojiweza kifedha na wazee.

Wakulima wamelalamikia ukawiaji katika usambazaji wa mbegu zisizotozwa malipo au za ruzuku wakati huu wa msimu wa upanzi.

Aidha, wanatoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo kuwapa mbolea ya kutumiwa katika shughuli ya upanzi.

Wakulima hao wakiongozwa na Mwakilishi Wadi wa zamani Teresa Lokichu wanatoa wito wa dharura kwa utawala wa Simon Kachapin kuwapa pembejeo hizo haraka iwezekanavyo.

Lokichu kadhalika ametoa wito kwa vituo vya usambazaji wa mbolea na mbegu kufunguliwa katika maeneo ya mashinani ili kuwapunguzia wakulima mzigo wa usafirishaji.

Joseph Sinen ni mzee kutoka eneo la Pokot Kaskazini. Amesema usambazaji wa mbegu za mahindi hasa kwa wazee na watu wasiojiweza katika jamii utawakinga dhidi ya njaa na utegemezi wa chakula cha msaada.

Share This Article