Wakulima ambao ni wanachama wa muungano wa jamii wa kutunza msitu ambao walikuwa wamepatiwa vipande vya ardhi ili kutekeleza kilimo katika eneo la Kithoka kwenye msitu wa lower Imenti wamelalamikia hatua ya waziri wa mazingira Soipan Tuya ya kuwataka waondoke kwenye eneo hilo.
Wakulima hao ambao pia wamejukumiwa kutunza sehemu hiyo ya msitu wanasema kwamba yatai walikuwa wametayarisha mashamba yao kwa ajili ya upanzi wa mimea ya chakula na miche ya miti wakati huu wa mvua lakini wameamuriwa waondoke.
Waahisi kwamba hatua ya waziri sio faafu kwa sababu lengo lao ni kurejesha sehemu hiyo ya msitu huku wakikuza chakula ili kuhakikisha familia zao zina chakula na mazingira yanafaidi.
Sasa wanataka waziri Tuya azuru eneo hilo binafsi ili kujifahamisha kikamilifu kuhusu mipango yao na labda kubadili mawazo kuwahusu.