Wakulima wadogo wa chai wanaowasilisha mazao yao kwa mamlaka ya ustawishaji chai nchini KTDA, watatejeshewa pesa walizokatwa kugharamia mbolea mwezi huu.
Awali KTDA ilikuwa imetoa arifa ya kuwarejeshea wakulima pesa hizo mwezi ujao.
Kulingana na arifa hiyo makato hayo yatajumuishwa katika mshahara wa mwezi Novemba, ambao wakulima watalipwa kufikia mwishoni mwa juma hili.
KTDA ilikuwa imeagiza metric tani
96,988 za mbolea mwaka huu, huku metric tani 8,000 za mwisho zikitarajiwa kusambaziwa wakulima wiki ijayo.