Wakili mkongwe Pheroze Nowrojee ameaga dunia

Tom Mathinji
1 Min Read
Wakili mashuhuri Pheroze Nowrojee, amefariki.

Kenya imempoteza wakili mkongwe Pheroze Nowrojee, aliyefariki leo Jumamosi akiwa na umri wa miaka 84.

Kifo cha Nowrojee kilitangazwa na mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Nchini (LSK) Faith Odhiambo, kupitia taarifa kwenye ukurasa wa X.

“Ni kwa huzuni kubwa Chama cha Wanasheria Nchini LSK, kinatangaza kifo cha mmoja wetu, Wakili Mkuu Pheroze Nowrojee,” alisema Odhimabo kwenye taarifa hiyo.

Licha ya kwamba alikuwa amestaafu miaka kadhaa iliyopita, Nowrojee alihutubia mkutano wa kila mwaka wa LSK Agosti mwaka 2024, ulioandaliwa Diani, kaunti ya Kwale.

Odhiambo alisema Nowrojee, alikuwa wakili mtulivu, mwenye  heshima, na aliyetumikia na kujitolea kutetea  haki.

Mawakili wengine pia walimuomboleza Nowrojee, wakimtaja mwenye tajiriba ya kupigiwa mfano, na inayopaswa kuigwa.

Mbunge wa Rarieda Otieno Amollo akimuomboleza Nowrojee alisema, “Nimehuzunika kupokea habari za kifo cha Pheroze Nowrojee, alikuwa wakili mpole aliyejitolea mahakamani. Pumzika pema Mkuu,”.

Wakili huyo alijitosa katika tasnia ya uanasheria mwaka 1965, na alikuwa  wakili wa Mahakama Kuu za Kenya, Tanzania na Zanzibar.

Website |  + posts
Share This Article