Wakfu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) umetoa dola milioni moja za Kimarekani, kama msaada wa kibinadamu kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Venezuela.
Pesa hizo zitasaidia kutoa huduma za dharura na misaada ya kibinadamu pamoja na kuwasaidia waathiriwa kuanza maisha upya.
Akitoa msaada huo, Rais wa FIFA Gianni Infantinho ,ametoa hakikisho la shirikisho hilo kusimama na binadamu wakati wa mikasa.
Shirikisho la soka nchini Venezuela (FVF), pia limekuwa mstari wa mbele kusimama na familia zilizoathiriwa na tetemeko hilo la ardhi.
Tangu kubuniwa kwake, Wakfu wa FIFA umetoa msaada wa mamilioni ya dola kuwasaidia waathiriwa wa mikasa.