Wakenya watamba barabarani

Dismas Otuke
1 Min Read

Daniel Ebenyo Simiu ameibuka mshindi wa makala ya mwaka huu ya mbio za umbali wa kilomita 25, akiweka rekodi mpya ya saa 1, dakika 11 na sekunde 13.

Mkenya mwingine Victor Togom amechukua nafasi ya pili kwa saa 1, dakika 11 na sekunde 26.

Daniel Ebenyo akishinda mbio za kilomita 25

Kwingineko, Gladys Chepkurui na Mathew Kimeli wametwaa ubingwa wa makala ya mwaka huu ya mbio za Bangsaen21 Half Marathon.

Chekurui ameshinda mbio za wanawake akitumia saa 1, dakika 9 na sekunde 46, akifuatwa na Sheila Chepkirui pia wa Kenya kwa saa 1, dakika 10 na sekunde 3, huku Angela Tanui akiridhia nafasi ya tatu kwa saa 1, dakika 11 na sekunde 8.

Matthew Kimeli ameshinda mbio za wanaume kwa saa 1, dakika 3 na sekunde 39, akifuatwa na Mwethiopia Tsegaye Getachew kwa saa 1, dakika 3 na sekunde 45, huku Amos Kipruto wa humu nchini akimaliza wa tatu kwa saa 1, dakika 3 na sekudne 52.

Share This Article