Wakenya waonywa dhidi ya kutumia viza za utalii kutafuta ajira ughaibuni

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imewaonya Wakenya dhidi ya kutumia viza za watalii kutafuta ajira ughaibuni, badala yake kuwataka kutumia njia halali za kusafiri nje ya nchi na kutafuta kazi.

Haya yamesemwa na Katibu katika Wizara ya Leba Shadrack Mwadime leo Jumatatu alipomtembelea Balozi wa Kenya mjini Ottawa, Kanada Carolyne Kamende Daudi..

Mwadime aliwataka Wakenya wanaotumia visa za watalii kukoma hulka hiyo akiongeza kuwa wengi wamepoteza pesa zao kutokana na stakabadhi zisizofaa.

Aidha, amewaonya mawakala wanaowahadaa Wakenya kwa kazi za ughaibuni na badala yake kuwatapeli, akisisitiza kuwa wataadhibiwa kisheria.

Aliongeza pia kuwa serikali itaanza mpango wa kuwapa kiinua mgongo Wakenya wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni ili kuwatosha.

Website |  + posts
Share This Article