Wakimbiaji wa Kenya wamezoa mataji ya wanaume na wanawake katika mbio za Suining Marathon katika mkoa wa Sichuan ulioko kusini magharibi mwa China.
Kyeva Cosmas Mutuku ameondoka na ushindi kwa kutumia muda wa saa 2:18:28 katika mbio za wanaume, na Gladys Jepkorir Kiprotich akinyakua taji la wanawake kwa saa 2:37:56.
Mwanariadha wa China Zhou Youfa ameshinda mbio za nusu marathon kwa wanaume, huku medali ya dhahabu kwa wanawake ikienda kwa Brigid Jelimo Kabergei wa Kenya.