Billy Mwangi, Peter Muteti, Rony Kiplagat na Benard Kavuli wameachiliwa huru baada ya kutekwa nyara majuma kadhaa yaliyopita na watu wasiojulikana.
Wanne hao walikuwa miongoni mwa watu 29 waliotoweka baada ya kutekwa nyara na watu wasiojulikana.
Billy ambaye ana umri wa miaka 24 ni mwanafunzi wa chuo na alipatikana mapema leo katika kaunti ya Embu huku Kiplagat akipatikana katika kaunti ya Machakos.
Muteti aliye na umri wa miaka 22 alitoweka tarehe 21 mwezi uliopita na amepatikana mapema leo katikati ya jiji la Nairobi.
Kavuli aliyetoweka kutoka Ngong amepatikana mjini Kitale.
Hata hivyo, baadhi ya familia za wanne hao zimesema waliopatikana baada ya kutekwa nyara hawakuwa katika hali nzuri kiakili.