Kinyume na hali ilivyokuwa siku 10 zilizopita barabara zote za kuingia na kutoka jijini Nairobi hazikuwa na msongamano leo.
Barabara zote zilikuwa nywee kinyume za siku nyingine za wiki kuashiria idadi kubwa ya watu tayari wamejiung na ndugu jamaa na rafiki kwa shamrasjamra za siku kuu ya Krismasi maeneo na mashambani au wamehiari kukaa majumbani hapa jijini.
Hali hii inatarajiwa kuendelea hadi wakati kusherehekea kuvuka mwaka mpya.
Msongamano mkubwa wa kuingia na kutoka jijini ilimekuwa ikishuhudia tangu wiki jana kutokana na idadi kubwa ya wasafiri na waliongia mjini kununua bidhaa kwa maandalizi ya Krismasi.