Wakenya milioni 5.4 wamethibitisha kulipa ushuru mwaka 2022 huku leo Ijumaa, Juni 30 ikiwa siku ya mwisho.
Kulingana na taarifa kutoka kwa mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini, KRA, kufikia Alhamisi, Juni 29, watu milioni 5.4 walikuwa wamejaza fomu za kuthibitisha kulipa ushuru kufikia saa moja usiku huku Ijumaa saa kumi alasiri ikiwa makataa.
KRA imesema kuwa watu waliothibitisha kujaza fomu za kulipa ushuru ni ongezeko la asilimia 16 zaidi ya idadi ya watu walioshiriki zoezi hilo kufikia Juni, 29 mwaka 2021.
Watu ambao hawatathibitisha kulipa ushuru kufikia Ijumaa saa kumi alasiri watatozwa faini.