Wakenya kuingia mbuga za wanyamapori bila malipo Septemba 28

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakenya wataingia hifadhi za wanyamapori bila malipo Septemba 28, katika madhimisho ya wiki ya wanyamapori ya shirika la Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Utalii na wanyamapori Rebecca Miano, ametawataka Wakenya kukumbatia fursa hiyo adimu na kuzuru mbuga za wanyamapori na kujifurahisha na kujiburudisha na kujielimisha.

Wiki ya wanyamapori nchini itaadhimishwa kuanzia Jumatatu Septemba 23, hadi Ijumaa tarehe 27, katika kaunti ya Kisumu.

Hafla hiyo itaongozwa na waziri wa Utalii Rebecca Miano.

Share This Article