Wakenya kuingia katika mbuga za kitaifa bila malipo

Tom Mathinji
1 Min Read

Waziri wa utalii Alfred Mutua ametangaza kwamba wakenya wataruhusiwa kuingia kwenye mbuga na makavazi ya kitaifa bila malipo siku ya Jamhuri.

Kwenye taarifa waziri alisema kuwa agizo hilo litawawezesha wakenya kujiburudisha.

Aliongeza kusema kuwa tangazo hilo pia linaambatana na sherehe za maadhimisho ya miaka 60 tangu Kenya ilipopata uhuru.

“Tunapoadhimisha miaka 60 tangu taifa hili kupata uhuru, serikali ina fahari kutangaza kuwa wakenya wataingia bila malipo katika mbuga zote za kitaifa siku ya Jamuhuri tarehe 12 mwezi Disemba,” alisema Waziri Mutua.

Agizo hilo la Mutua pia linajumuisha mbuga za majini na hifadhi za wanyama pori.

Kulingana na waziri wakenya wataruhusiwa kuingia kwenye maeneo hayo bila malipo kuanzia saa kumi na mbili alfajiri hadi saa kumi na mbili jioni.

Wakenya wanaonuia kufurahia toleo hilo watalazimika kuthibitisha utambulisho wao kupitia hati mbalimbali kikiwemo kitambulisho cha kitaifa nao watoto ni sharti waandamane na wazazi au watunzaji.

Maafisa wa shirika la huduma kwa wanyama pori nchini wametoa wito wa uvumilivu kwenye viingilio na ndani ya maeneo husika ili kuhakikisha huduma zinatekelezwa bila tatizo lolote.

TAGGED:
Share This Article