Wakenya 10,000 kusajiliwa kufanya ujenzi Dubai

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya Leba itaanza usaili na usajili wa Wakenya 10,000 watakaofanya kazi za ujenzi mjini Dubai.

Waziri wa Leba Afred Mutua ametanagaza kuwa uzajili huo utaanza leo kuendelea Jumamosi na kikamilika Jumapili katika chuo anuai cha kitaifa cha pwani.

Mchakato huo utaandaliwa kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kwa mjibu wa tangazo hilo kazi hizo zilizo ni Dubai ni za uashii,unajimu na wanaounganisha mabomba ya maji.

Walio na nia wanaombwa kufika wakiwa na vyeti vya masomo huku watakofaulu wakipata barua za mwaliko rasmi papo hapo.

Watakaopasi pia watapewa Visa za usafiri ndani ya siku tatu.

Usajili ulianzia katika kaunti ya Nairobi mwezi uliopita katika chuo anuai cha kitaifa Kabete na kile cha Nyeri .

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *