Huku taifa hili likiendelea kushuhudia mvua zinazosababishwa na hali ya El Nino, halmashauri ya kusimamia barabara kuu hapa nchini KeNHA, imewatahadharisha wananchi dhidi ya kutumia barabara iliyo katika eneo chepechepe la Kadzengo, katika kaunti ya Kilifi.
Kulingana na halmashauri hiyo, barabara hiyo imefurika kutokana na maji ya mvua kwa umbali wa zaidi ya mita 200.
KeNHA, imewaonya wananchi dhidi ya kutumia barabara hiyo, ikiwataka kusuburi hadi maji yapungue. Barabara hiyo kwa sasa inajengwa.
Barabara hiyo mpya itainuliwa kwa urefu wa mita 1.50, ili kuzuia viwango vya maji kufikia barabara.
Sehemu kadhaa za hapa nchini zimeathiriwa na mji ya mafuriko, huku watu wengi wakiachwa bila makao.