Wakazi wa Murang’a watakiwa kuwaunga mkono viongozi wao

Martin Mwanje
1 Min Read
Dkt. Stanley Kamau - Mkurugenzi Mkuu wa Ahadi Trust

Wakazi wa Murang’a katika eneo la Mlima Kenya wametakiwa kutowachukia viongozi wao waliochaguliwa na badala yake kufanya kazi nao kwa ajili ya maendeleo endelevu ya eneo hilo. 

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Ahadi Kenya Trust Dkt. Stanley Kamau amesema tangu kubanduliwa madarakani kwa Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachahua, baadhi ya viongozi hasa waliounga mkono kuondolewa kwa Gachagua hawajakuwa wakitembelea maeneo bunge yao.

Akizungumza katika soko la Rwathia katika eneo bunge la Kangema, Dkt. Kamau anasema hatua hiyo itapunguza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayopaswa kuwanufaisha wakazi.

“Tunahitaji kuepukana na siasa za chuki kwa sababu zitapunguza kasi ya maendeleo katika eneo hili,” alishauri Dkt. Kamau.

“Waruhusu wabunge waje katika maeneo yao na wapatiane msaada wa masomo kwa watoto wetu, wasimamie utekelezaji wa miradi ya maendeleo na wafahamu changamoto tunazopitia. Wacheni kuwafukuza.”

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *