Wakazi wa mtaa wa Maina mjini Nyahururu wapokea matibabu ya bure

Marion Bosire, Lydia Mwangi and Lydia Mwangi
1 Min Read

Wakazi wa mtaa wa Maina mjini Nyahururu, eneo bunge la Laikipia Magharibi kaunti ya Laikipia wamepokea huduma za matibabu bila malipo.

Mpango huo ambao ulijumuisha vipimo na matibabu uliandaliwa na muungano wa taasisi na vyuo vikuu vya eneo la Mlima Kenya kwa ushirikiano na hospitali ya Pearl na serikali ya kaunti ya Laikipia.

Lengo la waandalizi wa mpango huo ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, sambamba na mpango wa serikali.

Daktari Benard Karanja alihutubia wanahabari ambapo alitambua juhudi za serikali katika sekta ya afya akisema ili mafanikio zaidi yapatikane, jamii zinazoisho katika mitaa ya mabanda ni lazima zihamasishwe.

Alisema vituo vya afya na huduma za afya lazima pia zipelekwe karibu na wakazi wa maeneo hayo, kwa sababu wengi wanaishi maisha ya uchochole.

Karanja aliwataka wadau wa kibinafsi washirikiane na wahudumu wa afya ya jamii kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wote kwa sababu serikali peke yake haiwezi kuafikia hilo.

Usemi huo ulikaririwa na Daktari Robert Mbugua msimamizi wa hospitali ya Pearl na Esther Wairimu mhudumu wa afya ya jamii anayeshughulikia eneo hilo na Maina.

Website |  + posts
Share This Article