Wakaguzi wa CAF wazuru Kenya kutathmini matayarisho ya CHAN

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa shirikisho la soka barani Afrika -CAF,waliwasili nchini jana kufanya ukaguzi wa miundo msingi ya Kenya kwa maandalizi ya fainali za Kombe la CHAN ,Februari mwakani.

Ujumbe huo wa CAF unazuru Kenya baada ya kukamilisha ukaguzi wa Uganda na Tanzania ambao pia wataandaa fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanasoka wa ligi za nyumbani CHAN kwa pamoja na Kenya.

Viwanja vinavyopaniwa kutumika kwa maandalizi ya fainali za CHAN nchini Kenya ni Nyayo na Kasarani.

Uwanja wa Nyayo umefanyiwa ukarabati mdogo licha ya kufungwa kwa muda mrefu huku ule wa Kasarani ,ukitarajiwa kuwa tayari mwishoni mwa mwezi ujao ,kwani unafanyiwa ukarabati mkubwa.

Kuna hofu ya kuwa huenda Kenya ikakosa kuwa tayari kuandaa michuano ya CHAN ikizingatiwa kuwa hadi sasa haina hata uwanja mmoja ulio tayari, wakati Uganda ikiwa  imekamilisha uwanja wa Nelson Mandela nao Tanzania uwanja wa Benjamin Mkappa .

Mataifa hayo matatu yatatumia CHAN kujipima kwa maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 .

Ukaz

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *