Wagonjwa wa macho Kisumu wanufaika kwa msaada wa upasuaji

Dismas Otuke
1 Min Read

Zaidi ya wagonjwa 1,000 wamenufaika katika uchunguzi na matibabu ya bure ya macho na upasuaji mjini Kisumu katika kambi inayodhaminiwa na kampuni ya huduma ya jamii ya Pankaj na hospitali ya mafunzo na rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH).

Shughuli hiyo ilianza wiki jana kwenye maeneo bunge yote saba ya kaunti ya Kisumu na inatarajiwa kuwafaidi zaidi ya wagonjwa 600.

Kwa mujibu wa naibu wa gavana wa kaunti hiyo, Dk.Mathews Owili, kambi hiyo itawafaidi wengi wasio na uwezo wa gharama za matibabu. Pia alishukuru Pankaj kwa msaada huo na kuongeza kuwa serikali yake itazidi kushirikiana na mashirika mengine ili kufikia wagonjwa wenye mahitaji ya huduma hiyo.

Naye mkurugenzi mkuu wa JOOTRH Dk.Richard Lesiyampe, aliisema kuwa huduma hiyo inayojumuisha usafirishaji wa wagonjwa kutoka nyumbani hadi hospitalini humo kwa matibabu maalum, imewapa wagonjwa hao tumaini la kuona tena.

Alifichua kuwa upasuaji wa jicho ( cataract Surgery) hugharimu shilingi 15,000 ambazo wagonjwa wengi hushindwa kumudu.

Kambi hiyo itafungwa ijumaa huku tayari upasuaji 24 wa ubongo na uti wa mgongo ukiwa umefanyika vyema.

Share This Article