Wafugaji Mogotio wapinga mpango wa kufungua tena kituo cha kuchinjia punda

Martin Mwanje
1 Min Read

Kufunguliwa tena kwa kituo cha uchinjaji wa punda katika eneo bunge la Mogotio, kaunti ya Baringo kutaongeza uhalifu hasa wizi wa punda.

Mamia ya wakulima na wafugaji wa punda kadhalika wanasema hatua hiyo itakuwa chanzo cha laana kwa jamii.

Waliyasema hayo walipoandamana katika eneo la Maji Mazuri kulaani kufunguliwa tena kwa kituo hicho wanachodai pia kitasababisha kupotea kwa ajira.

Wakiongozwa na mzee kutoka jamii ya Lembus, Samuel Kiragu, wamesema yeyote atakayechinja punda atapata laana inayoweza hata ikasababisha kifo.

Walikashifu matamshi ya Waziri wa Kilimo, Mithika Linturi kuhusu kufunguliwa tena kwa kituo hicho.

Kwa upande wake, Josephine Kinangai, ambaye ni mtetezi wa punda, amesema mnyama huyo huchangia pakubwa kwa kazi za nyumbani, mbali na kusomesha wanao hadi Chuo Kikuu.

Sasa wanawataka viongozi wa kitaifa na kaunti hiyo kuingilia kati.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *