Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets, ilitoka sare tasa na Tunisia leo kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ya kufuzu kwa fainali za kuwania kombe la mataifa Afrika mwaka ujao.
Warembo hao wa nyumbani sasa wana kibarua kigumu jijini Tunis Februari 26, katika mechi ya marudiano kuandikisha ushindi ili wafuzu kwa raundi ya pili.
Starlets walikuwa na nafasi kochokocho za kutikisa wavu wa Tunisia katika mechi hiyo iliyochezewa katika uwanja wa Ulinzi, lakini juhudi zao ziliambuliwa patupu, huku timu hizo mbili zikiridhika na sare tasa.
Iwapo Starlets watafuzu kwa raundi ya pili, basi watakutana na Niger au Gambia mwezi Oktoba mwaka huu, Na ikiwa itafuzu katika raundi ya pili, itajikatia tiketi ya kuwania kombe la akina dada Barani Afrika(WAFCON), nchini Morocco mwaka ujao.
Fainali za WAFCON 2026 nchini Morocco, zitajumuisha timu 12.