Wafanyakazi wa kampuni ya KEWASCO wagoma

Tom Mathinji
1 Min Read

Wafanyakazi wa kampuni ya maji na usafi (KEWASCO) kaunti ya Kericho, wamesusia kazi wakidai hawajapokea mshahara kwa muda wa miezi 17, ambazo ni jumla ya shilingi milioni 177.

Kulingana na Katibu Mkuu wa chama cha wafanyikazi wa KEWASCO Tom Emober, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Erick Siele, amewavunja moyo wafanyakazi kupitia uongozi wake usio na tajiriba na utaalam.

Wafanyakazi hao, walitoa wito kwa Mkurugenzi huyo Mkuu kujiuzulu kwa kushindwa kuwashughulikia wafanyakazi hao ambao wengine wamelazimika kuuza mali yao, ili kulipa mokopo ya benki.

Mwakilishi wadi ya Kibchebor Erick Bett, alilaumu uongozi mbaya wa mkurugenzi huyo. ambao umesababisha kudororra kwa kampuni hiyo  tangu mwaka 2022.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *