Waendeshaji magari watakiwa kuwa waangalifu msimu huu wa sherehe

Martin Mwanje
2 Min Read
Douglas Kanja - Inspekta Mkuu wa Polisi

Waendeshaji magari wametakuwa kuwa waangalifu zaidi na kuzingatia sheria za barabaranai wakati pirikapirika za msimu wa sherehe za Sikukuu ya Krimasi na Mwaka Mpya zikishika kasi. 

Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja amelalamikia idadi ya ajali ambazo hushuhudiwa wakati wa msimu huu, ajali anazosema husababishwa na kutomakinika kwa madereva.

“Kwa kuzingatia data zetu, ajali za barabarani zinasalia kuwa chanzo kikuu cha majeraha na vifo nchini mwetu. Ilhali, nyingi ya ajali hizi husababishwa na vigezo vya kibinadamu vinavyoweza kuepukika hasa kutozingatia sheria za barabarani,” amelalama Kanja kupitia taarifa.

“Ni wazi kwamba ajali za barabarani huongezeka wakati wa misimu ya sherehe, na tayari, tunashuhudia ongezeko la ajali za barabarani mwaka huu.”

Kulingana na Kanja, kuanzia mwezi Januari hadi Novemba mwaka jana, vifo 3,469 vilivyotokana na ajali za barabarani viliripotiwa ikilinganishwa na vifo 3,681 vilivyoripotiwa mwaka huu, likiwa ni ongezeko la vifo 212.

Vile mwaka 2023, watu 20,239 walijeruhiwa kutokana na ajali za barabarani ikilinganishwa na watu 21,620 mwaka huu, likiwa ni ongezeko la watu 1,381.

Inspeka Mkuu huyo wa Polisi anasema ili kukabiliana na visa hivi, Wakenaya watashuhudia ongezeko la maafisa wa polisi barabarani kote nchini wakati wa msimu huu wa sherehe za Krimasi na Mwaka Mpya.

Maafisa kutoka vikosi maalum na wale waliovalia mavazi ya raia ni miongoni mwa watakaotumwa kushika doria barabarani.

“Ingawa Huduma ya Taifa ya Polisi imeweka hatua hizi madhubuti ili kuhakikisha usalama, ningependa kuwakumbusha Wakenya wote kwamba usalama na usalama wa barabarani ni jukumu letu sote,” alimalizia Kanja.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *