Wacheni siasa za mapema, arai Gavana wa West Pokot

Martin Mwanje & Stephen Aengwo
1 Min Read
Simon Kachapin - Gavana wa West Pokot
Gavana wa kaunti ya West Pokot Simon Kachapin ametoa wito kwa wanasiasa kusitisha kampeni za mapema na badala yake kuwatumikia Wakenya.
Kachapin amesisitiza umuhimu wa viongozi wote waliochaguliwa kutoa kipaumbele kwa utekelezaji wa miradi ya maeneleo kwa manufaa ya raia.
Akizungumza katika eneo la Sigor, Kachapin alisema inasikitisha kwamba miaka 60 baada ya Kenya kujinyakulia uhuru, nchi hii bado inategemea misaada.
Awali, wito sawia ulitolewa na viongozi wa kidini wanaowataka wanasiasa kupunguza joto linalopanda la kisiasa nchini na badala yake kutekeleza miradi ya maendeleo itakayowafaidia Wakenya.
Wanatoa mfano wa changamoto mbalimbali zinazowakumba Wakenya ikiwa ni pamoja na gharama ya juu ya maisha na ukosefu wa ajira.
Matamshi ya Gavana Kachapin yanakuja wakati ambapo wanasiasa wameanza kunoa makali ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 huku miungano ya kisiasa ikianza kuundwa.
Imesalia miaka miwili kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu ujao na kuna mashaka kwamba mipango ya maendeleo huenda ikapewa kisogo wakati wanasiasa wakigeukia njama za kutetea nyadhifa zao.
Martin Mwanje & Stephen Aengwo
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *