Naibu Rais Rigathi Gachagua, ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kupunguza joto la kisiasa, na badala yake kuangazia utoaji huduma kwa wananchi.
Gachagua aliwataka alisema ataendelea kufanya kazi na viongozi wote bila kujali miegemeo yao ya kisiasa au maeneo wanakotoka, ili kuhakikisha maendeleo ya taifa hili.
Naibu huyo wa Rais aliwataka wakazi wa Mlima Kenya kudumisha umoja, huku akiwanyooshea kidole cha lawama baadhi ya wanasiasa wanaotaka kugawnya eneo hilo kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007.
“Wale ambao wanataka kugawanya eneo la Mlima Kenya hawatafaulu. Mpango huo hautafuadafu kwa sababu wakazi wa eneo hilo wanataka kuishi kwa umoja,” alisema Gachagua.
Akizungumza mjini Limuru kaunti ya Kiambu leo Jumamosi, naibu huyo wa Rais, aliwalaumu baadhi ya wanasiasa kwa kupandisha joto la kisiasa hapa nchini.
“Tunawahimiza wabunge kupunguza joto la kisiasa na kuwahudumia wakenya. Wakenya hawataki siasa, lakini huduma kutoka kwa serikali,” aliongeza Gachagua.
Alisema ni miaka miwili tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022, na hivyo siasa hazina nafasi wakati huu.