Wabunge watano ‘waasi’ watimuliwa na ODM

Dismas Otuke
1 Min Read
Wabunge wa ODM walikpokuana na Rais Ruto Ikuluni

Kamati kuu ya chama cha ODM imeafikia uamuzi wa kuwatimua wabunge watano ‘waasi; waliokiuka itikadi za chama.

ODM imesema imewatimua wabunge hao kwa utovu wa nidhamu baada yao kuhiari kushirikiana na muungano wa Kenya Kwanza bila idhini ya chama.

Wajumbe waliopigwa teke ni pamoja na Felix Odiwuor wa Lang’ata, Seneta wa Kisumu Profesa Tom Ojienda, mbunge wa Gem Elisha Odhiambo, Gideon Ochanda wa Bondo na mbunge waSuba  Kusini Caroli Omondi.

Omondi tayari amekaidi akisema kamwe hataomba msamaha na pia hahitaji kutetea kiti chake kwa tiketi ya chama cha ODM ili kukihifadhi wakati wa uchaguzi wa mwaka 2027.

Wanachma hao waliapa kufanya kazi na serikali ili kunufaika na miradi ya maendeleo katika maeneo yao ya uwakilishi.

Website |  + posts
Share This Article