Spika wa Bunge la Kiataifa Moses Wetangula ameitisha kikao maalum Mei 13 kubaini hatma ya Waziri wa Kilimo Mithika Linturi.
Wabunbe wamo kwenye likizo ndefu baada ya vikao kusitishwa wiki iliyopita na wanatarajiwa kurejea Juni 4 mwaka huu kwa vikao.
Kamati ya bunge ya wanachama 11 iliteuliwa wiki iliyopita kumchunguza Linturi baada ya bunge kupitisha hoja ya kutokuwa na imani naye kufuatia sakata ya mbolea ghushi.
Kamati hiyo inaongozwa na mwakilishi wanawake wa kaunti ya Marsabit Naomi Waqo na ilianza vikao vyake Alhamisi iliyopita huku ikiwa na muda wa siku 10 kukamilisha shughuli zake.
Wakati wa vikao vyake kamati hiyo itawasikiza mashahidi huku pia waziri akipewa fursa ya kujitetea.
Wabunge 149 walipiga kura ya kuunga mkono mswaada huo uliowasilishwa na mbunge wa Bumula Wamboka Waanami wa kutimuliwa kwa Linturi, huku wengine 36 wakipinga na watatu wakakosa kupiga kura.