Wabunge wameitaka serikali kuwaajiri Walimu wanagenzi wa shule za Junior Secondonary, kwa mkataba wa kudumu ili kuimarisha utendakazi wao.
Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro,mwenzake wa Marakwet magharibi Timothy Toroitich na mwakilishi wanawake wa kaunti ya Narok Rebecca Tonkei,wameitaka tume ya kuajiri walimu nchini TSC, kuwapa walimu wanagenzi wa Junior secondary chini-JSS kwa mikataba wa kudumu.
Wakizungumza mjini Narok, Tonkei alisema walimu hao wanalipwa kiwango cha chini cha pesa kwa sasa na kuwapa mikataba ya kudumu kutawawezesha kupokea malipo mazuri na kuwamotisha.
Kando na hayo Nyoro pia ameitaka TSC kuajiri walimu 20,000 mwaka ujao wa fedha.
Toroitich kwa upande wake aliishauri TSC kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama, uliositisha uajiri wa wanagenzi hao kwa mkataba wa kudumu.