Wabunge wanapanga kuwasilisha mswaada bungeni wa kumng’atua mamlakani waziri wa kilimo Mithika Linturi Juma lijalo.
Yamkini mswaada huo tayari unaungwa mkono na Wabunge zaidi ya 70 .
Njama ya kumtimua Linturi ofisini inatokana na sakata ya mbolea ghushi iliyouziwa wakulima huku wabunge wakihoji ufaafu wake kwenye wizara hiyo.
Mswaada huo unapanga kuwasilishwa Bungeni Jumanne Ijayo na Mbunge wa Mbeere Kaskazini Geofrey Ruku.
Wabunge pia wanapanga kuwasilisha mswaada mwingine wa kutokuwa na imani na waziri wa Afya Susan Nakhumicha kwa kushindwa kutatua mgomo wa Madaktari ambao umeingioa siku ya 31.