Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, EALA sasa watakuwa wakilipwa na mabunge yao husika.
Hatua hiyo itaanza kutekelezwa katika bunge lijalo.
“Wabunge wa EALA wanaowakilisha nchi zao tofauti, ambao kwa sasa wanatumia asilimia 30 ya bajeti ya EAC, kuanzia bunge lijalo watalipwa mishahara yao na mabunge yao husika,” alitangaza Rais William Ruto.
Aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa Kawaida wa 25 wa Wakuu wa Nchi uliofanyika mjini Arusha nchini Tanzania leo Jumamosi na kuhudhuriwa na Marais wengine sita kutoka jumuiya hiyo.
Hatua hiyo nayo inakuja wakati ambapo kumekuwa na ripoti za wabunge wa EALA kutolipwa mishahara yao kwa hadi kipindi cha miezi mitatu.
Ni hali inayotokana na kukosa kwa nchi wanachama kutoa michango yao kwa EAC wakati unaofaa.
Ruto, ambaye ni mwenyekiti anayeondoka wa jumuiya hiyo, pia amesema maamuzi ya EAC kuanzia sasa yatakuwa yakifanywa kupitia makubaliano au asilimia 65 ya wanachama.
Awali, maamuzi hayo yalihitaji kufanywa