Orodha ya wanandinga wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Afrika mwaka huu imetangazwa.
Baadhi ya walioteuliwa ni pamoja na washindi wa mwaka uliopita Sadio Mane wa Senegal na Asisat Oshaola wa Nigeria kwa wanaume na wanawake mtawalia.
Wachezaji 30 wameteuliwa kuwania tuzo kuu ya wanaume ,wengine 20 wanawania tuzo ya mchezaji bora katika mashindano ya vilabu ,kocha bora wa mwaka,Klabu bora ya mwaka na timu bora ya taifa pamoja na mchezaji chipukizi bora wa mwaka.
Pia kwa mara ya kwanza CAF imeanzisha tuzo ya kipa bora barani Afrika kwa wale wanaosakata soka Afrika kwa wanaume na wanawake.
Baadhi ya wanandinga waliojumuishwa katika orodha ya 30 bora wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa mwaka ni Ramy Bensebaini wa Algeria na klabu ya Borusia Dortmund,Riyad Mahrez wa Algeria na klabu ya Al Ahli,Edmond Tapsoba wa Burkina Faso na Bayer Leverkusen ,Andre-Frank Zambo Anguissa wa Cameroon na SSC Napoli na Vincent Aboubacar kutoka Cameroon na klabu ya Besiktas.
Wengine katika orodha ni Mohamed ElShenawy wa Misri na Al Ahly ,Thomas Partey wa Ghana na Arsenal ,Achraf Hakimi wa Morocco na Paris Saint-Germain,Azzedine Ounahi wa Morocco na Olympique Marseill,Hakim Ziyech wa Morocco na Galatasaray,Sofyan Amrabat wa Morocco na Manchester United na Victor Osimhen wa Nigeria na klabu ya Napoli.
Washindi watabainika kwenye halfa itakayoandaliwa mjini Marrakech Morocco Disemba 11.