Waakilishi wadi 11 wa UDA kutoka Uasin Gishu watupwa nje

Dismas Otuke
1 Min Read

Waakilishi wodi 11 wateule wa chama cha United Democratic Alliance( UDA) wamepoteza viti vyao katika bunge la kaunti ya Uasin Gishu baada ya mahakama ya kuu kudumisha uamuzi wa kuwapokonya viti kwa kutilia shaka uteuzi wao.

Kulingana na uamuzi huo mahakama iliikosoa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kwa kuwasilisha orodha iliyokuwa na majina hayo 11 licha ya jopo la chama kuwakana.

Hatua hii ina maana kuwa waakilishi wodi hao ambao walikuwa wameteuliwa na chama watalazimika kutupwa nje na chama kuwateua wengine.

 

TAGGED:
Share This Article